2 Timothy 2:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Endelea kuwakumbusha mambo haya, ukiwaonya mbele za Mungu waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote, bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Endelea kuwakumbusha watu juu ya mambo haya. Waonye kwa mamlaka mbele za Mungu wasipigane juu ya maneno. Mapigano hayo hayana mambo mazuri, bali huwaharibu wanaoyasikiliza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakumbushe watu wako mambo haya, na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yo yote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana Isa waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wanaoyasikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakumbushe mambo hayo na kuwaonya mbele yake Mungu, wasibishane! Maana haifai kitu, huwapotoa tu wenye kusikiliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwakumbushe watu maneno hayo yote na kuwaonya wazi mbele ya Mungu waache kubishana juu ya maneno. Mabishano hayana faida kwa maana yanawapoteza wale wanaoyasikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.