2 Timothy 2:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kupita, nao hupindua imani ya baadhi ya watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
aliyeiasi na kuikosa kweli. Wanasema kuwa ufufuo kutoka kwa wafu kwa watu wote umekwisha kutokea, na wanageuza imani za watu wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kuwako na kupotosha baadhi ya watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kuwako, nao huharibu imani ya baadhi ya watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
waliopotelewa nayo yaliyo ya kweli wakisema: Ufufuko umekwisha kuwapo. Ndivyo, walivyokosesha hata wengine, wasimtegemee Bwana tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao wamepotoka mbali na ukweli, wamepotosha imani ya watu wengi wakisema kwamba ufufuko tunaongojea umekwisha kufanyika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
walioikosa kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, nao waipindua imani ya watu wengine.