2 Timothy 2:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Mwenyezi Mungu anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Mwenyezi Mungu na auache uovu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hata hivyo, msingi ulio imara ambao Mungu aliuweka unasimama imara, na maneno haya yameandikwa juu yake: “Bwana anawajua wale walio wake,” na “Kila anayesema kuwa ni wa Bwana aweze kuuacha ubaya.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini msingi wa Mungu ulio madhubuti umesimama ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake” tena, “Kila alitajaye jina la Bwana auache uovu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini msingi wa Mwenyezi Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana Mwenyezi anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana Mwenyezi, na auache uovu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini msingi, Mungu aliouweka, uko, umeshupaa vivyo hivyo, hujulikana kwa muhuri yake, ni hii: Bwana huwatambua walio wake! Tena: Kila mwenye kulitambikia Jina la Bwana atenguke penye upotovu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini musingi uliojengwa na Mungu, unasimama imara. Nayo maneno haya yamechapwa juu ya musingi ule “Bwana anajua wale wanaokuwa wake,” na haya mengine: “Kila mutu anayesema kwamba yeye ni wa Bwana anapaswa kujitenga na maovu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.