2 Timothy 2:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndani ya nyumba kubwa hakuna vyombo vya dhahabu na fedha pekee, bali hata vya udongo na mbao. Na vingine ni vya kutumika kwa matukio maalumu, na vingine ni kwa matumizi ya kawaida.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo, vingine kwa matumizi maalum na vingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika nyumba kubwa hamna vyombo vya dhahabu au vya fedha tu, ila vimo hata vyombo vya miti na vya udongo; navyo vingine ni vya mapambo, vingine ni vya machafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndani ya nyumba kubwa, hamuna vyombo vya zahabu na feza tu, lakini muko vilevile vyombo vya miti na vya udongo. Vimoja ni vya matumizi ya kipekee na vingine ni vya matumizi ya kawaida.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi katika nyumba havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina heshima.