2 Timothy 2:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa unajua hayo huzaa magomvi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nyakati zote ujiepushe na mabishano ya kijinga, kwa sababu unajua kuwa huleta mabishano makubwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo ya elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mabishano ya upuzi wa watu wasioonyeka yakatae! Jua, ya kuwa huleta magombano tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ukatae mabishano ya kipumbafu na yasiyokuwa na maana; unajua wewe mwenyewe kwamba yanaleta magomvi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi: