2 Timothy 2:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena haimpasi mtumishi wa Bwana Isa kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwani mtumwa wa Bwana hapaswi kubishana, bali kuwa mkarimu kwa watu wote, mwenye ujuzi katika kufundisha na asiye mtukanaji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena haimpasi mtumishi wa Bwana Isa kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini aliye mtumwa wa Bwana haimpasi kugombana, sharti awaendee wote kwa unyenyekevu akijua kuwafundisha, akivumilia wenye uovu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mutumishi wa Bwana hapaswi kugombana. Anapaswa kuwa mupole kwa watu wote, anayejua kufundisha na muvumilivu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,