2 Timothy 2:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, mwanariadha hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kama kuna mtu anayeshiriki katika mashindano ya riadha, hawezi kushinda taji endapo hatashindana kwa kufuata sheria.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtu angawa anashindana, hafungwi kilemba asiposhinda kikweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile mutu yeyote anayeshindana katika michezo hawezi kupata zawadi ya ushindi kama asipotii kanuni za michezo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta mtu akishindana hapewi taji asiposhindana kwa halali.