2 Timothy 3:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
udhalimu na mateso. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana Isa aliniokoa katika hayo yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
mateso yangu na taabu zangu. Mnayajua mambo yaliyonitokea kule Antiokia, Ikonia, na Listra, mateso ya kutisha niliyoyastahimili! Lakini Bwana akaniokoa kutoka katika hayo yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
udhalimu na mateso. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mateso na taabu, yaani, yale mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana Isa aliniokoa katika hayo yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
udhalimu na mateso. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hata mafukuzo na mateso yangu, niliyoyapata huko Antiokia na Ikonio na Listra. Nami niliyavumilia hayo mafukuzo yote, naye Bwana akaniokoa katika yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mateso na taabu yangu. Unajua mambo yote ambayo yalinitokea kule Antiokia, Ikonio na Listra. Mateso haya niliyavumilia, na Bwana akaniokoa katika yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.