2 Timothy 3:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na jinsi tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kupitia kwa imani katika Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na unajua kwamba umeyajua Maandiko Matakatifu tangu ukiwa mtoto. Maandiko hayo yana uwezo wa kukupa hekima. Hekima hiyo itakuongoza hadi kwenye wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakumbuka kwamba tangu utoto wako umejua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwa sababu umeyajua Maandiko matakatifu tangu utoto wako, haya yanaweza kukuerevusha, uokoke kwa kumtegemea Kristo Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, tangia utoto wako unajua Maandiko Matakatifu yanayoweza kukupatia hekima kusudi uokolewe kwa njia ya kumwamini Kristo Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.