2 Timothy 3:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose. Hao ni watu wa akili potovu na imani ya uongo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo watu hawa hupingana na kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama ambavyo Yane na Yambre walivyompinga Musa, ndivyo hata watu hawa wanavyoipinga kweli. Ni watu ambao akili zao zimeharibika, nao wameshindwa kuifuata imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose. Hao ni watu wa akili potovu na imani ya uongo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Mose, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose. Hao ni watu wa akili potovu na imani ya uongo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Yane na Yambure waliombisha Mose, ndivyo, hata hao wanavyoyabisha yalio ya kweli; hufanana nao wenye wazimu, wakajulika kuwa wenye kumtegemea Mungu bure tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wale wanapinga ukweli kama vile Yane na Yambure walivyopingana na Musa. Akili ya watu hao imepotoka, nayo imani yao imegeuka bure.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vile vile kama Yanne na Yambre walivyopingana na Mnsa, vivyo hivyo na hawa wapingana na kweli, ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.