2 Timothy 3:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile upumbavu wa hao watu wawili ulivyokuwa dhahiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hawataendelea mbele zaidi, kwa sababu upumbavu wao utadhihirika wazi wazi kwa watu wote, kama ujinga wa Yane na Yambre ulivyojulikana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hawataendelea sana, kwani upumbavu wao utawatokea wote waziwazi, kama hata upumbavu wao wale ulivyojulika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hawataendelea mbali sana, kwa sababu upumbafu wao utaonekana wazi mbele ya watu wote, sawa ilivyokuwa kwa Yane na Yambure.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama na wa hao ulivyokuwa.