2 Timothy 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa nimewekewa taji la haki ambalo Bwana, Mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa tuzo ya mshindi inaningoja, hii ni taji inatolewa kwa wenye haki. Bwana, aliye hakimu wa haki atanipa taji hiyo katika Siku ile. Ndio atanipa mimi na yeyote mwingine anayengojea kwa dhati kuja kwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile, wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lisaalo ni kufungwa kilemba kipasacho waongofu, nilichowekewa nami Siku ile nitakipata kwake Bwana aliye mhukumu mwenye kweli; lakini si mimi tu atakayekipata, ila nao wote waliokuwa wamempenda, atokee waziwazi.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangia sasa nimetayarishiwa zawadi ya ushindi, ndiyo ile taji ya haki, ambayo Bwana anayekuwa Mwamuzi wa haki atakayonipa siku ile ya kurudi kwake. Wala hatanipa mimi peke yangu tu, lakini na wale wote wanaopenda kumwona wakati atakaporudi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.