3 John 1:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa waumini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nitakapokuja, nitaongea naye mbele ya kanisa juu ya hiki anachokifanya. Anadanganya na kusema mambo mabaya juu yetu, lakini hayo siyo yote. Anakataa kuwapokea na kuwasaidia wanaoamini wanaosafiri kwenda huko. Na hawaruhusu watu wengine kuwasaidia. Kama wakifanya hivyo, anawazuia wasikusanyike na kanisa tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuzia nje ya kanisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo kama nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke kanisani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo kama nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa kundi la waumini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuza nje ya kanisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nitakapokuja nitazikumbusha kazi zake, anazozifanya akituteta sisi kwa maneno mabaya. Nayo hayo hayamtoshi: mwenyewe hawapokei ndugu, nao wanaotaka kuwapokea huwazuia, kisha huwafukuza kwenye wateule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo wakati nitakapokuja, nitaonyesha wazi mambo yote anayotenda akitusingizia sisi maneno mabaya. Lakini hatosheki na mambo yale, yeye mwenyewe anakataa kukaribisha wandugu wale wanaokuwa katika safari. Na wale wanaotaka kuwakaribisha, anawakataza na kuwafukuza katika kanisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.