3 John 1:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema anatoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Rafiki yangu mpendwa, usiige lililo baya; bali iga lililo jema. Yeyote anayetenda yaliyo mema hutoka kwa Mungu. Ila yeyote anayetenda maovu bado hajamjua Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpenzi, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Ye yote atendaye mema atoka kwa Mungu, atendaye mabaya hakumwona Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mwenyezi Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpendwa, usiuige uovu, ila uuige wema! Anayefanya yaliyo mema ni wa Kimungu; anayefanya yaliyo maovu hakumwona Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mupendwa wangu, usifuate mufano mubaya, lakini ufuate mufano muzuri. Mutu anayetenda mema ni mutoto wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hashirikiani na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.