3 John 1:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakashuhudia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza kuhusu uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya waamini walikuja na kunieleza juu ya kweli iliyo katika maisha yako. Waliniambia kuwa unaendelea kuifuata njia ya kweli. Hili lilinifanya nijisikie furaha sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakaiambia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakashuhudia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza juu ya uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nilifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakashuhudia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nalifurahi sana, ndugu walipokuja na kutushuhudia, kuwa u mwenye kweli, kama wewe unavyoishika njia ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilifurahi sana wakati wandugu wamoja walipofika na kunielezea juu ya ukweli unaokuwa ndani yako na kwamba unaishi katika ukweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama nendavyo katika kweli.