3 John 1:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nililiandikia kundi la waumini, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Niliandika barua kwa kanisa, ila Diotrefe hasikilizi yale tunayosema. Yeye daima anataka kuwa kiongozi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nililiandikia kanisa, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nililiandikia kundi la waumini, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nililiandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yako mengine, niliyoyaandikia wateule. Lakini Diotirefe anayependa kuwa mkubwa wao hatusikii sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimeandikia kanisa maneno machache lakini Diotrefe, anayependa kuwa musimamizi wao, anakataa kututii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Naliliandikia kanisa, lakini Diotrefe apendae kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.