Acts 1:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka ule mlima uitwao Mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato kutoka mjini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo mitume walirudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, ulio umbali wa kama kilomita moja kutoka Yerusalemu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka ule mlima uitwao Mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato kutoka mjini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato kutoka mjini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mitume wakarudi Yerusalemu kutoka ule mlima uitwao Mlima wa Mizeituni ulioko karibu kilomita moja kutoka mjini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipoondoka penye huo mlima unaoitwa Wa Michekele, ulioko karibu ya Yerusalemu, ni mwendo usio na mwiko wa siku ya mapumziko; wakarudi Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mitume wakarudi Yerusalema tokea kwenye mulima wa Mizeituni unaokuwa karibu na muji huo kwenye umbali wa yapata kilometre moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kiisha wakarudi kwenda Yerusalemi kutoka mlima ulioitwa wa mizeituni, ulio karibu na Yerusalemi, wapata mwendo wa sabato.