Acts 1:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akasema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu nguvuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndugu zangu, ilibidi andiko litimie, ambalo Roho wa Mungu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda, aliyewaongoza wale waliomkamata Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Kaka na dada zangu, katika Maandiko Roho Mtakatifu alisema kupitia Daudi kwamba jambo fulani lazima litatokea. Alizungumza kuhusu Yuda, yule aliyekuwa katika kundi letu wenyewe. Yuda alihudumu pamoja nasi. Roho alisema Yuda atawaongoza watu kumkamata Yesu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akasema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu nguvuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akasema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu nguvuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndugu zangu, ilibidi maandiko yatimie yale ambayo Roho Mtakatifu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndugu zangu, ilibidi Andiko litimie ambalo Roho wa Mwenyezi Mungu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akasema, “Ndugu zangu, ilikuwa lazima ile sehemu ya Maandiko Matakatifu itimie, sehemu ambayo Roho Mtakatifu, kwa maneno ya Daudi, alibashiri habari za Yuda ambaye aliwaongoza wale waliomtia Yesu nguvuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waume ndugu zangu, ilipasa andiko litimie, Roho Mtakatifu alilolisema kale kinywani mwa Dawidi kwa ajili ya Yuda aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yasu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wandugu zangu, ilikuwa lazima yale Maandiko Matakatifu yatimie ambayo Roho Mutakatifu alitabiri kwa kinywa cha mufalme Daudi juu ya Yuda, yule aliyewaongoza wale waliomukamata Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,