Acts 1:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: ‘Makao yake yabaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake.’ Tena imeandikwa: ‘Mtu mwingine achukue nafasi yake ya huduma.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Zaburi, “ ‘Mahali pake na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi humo,’ na, “ ‘Mtu mwingine aichukue nafasi yake ya uongozi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akasema, “Katika kitabu cha Zaburi, jambo hili limeandikwa kuhusu Yuda: ‘Watu wasipakaribie mahali pake; Yeyote asiishi hapo.’ Pia imeandikwa kuwa: ‘Mtu mwingine achukue kazi yake.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: Nyumba yake ibaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake. Tena imeandikwa: Mtu mwingine achukue nafasi yake katika huduma hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: ‘Makao yake yabaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake.’ Tena imeandikwa: ‘Mtu mwingine achukue nafasi yake ya huduma.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama vile ilivyoandikwa katika kitabu cha Zaburi, “ ‘Mahali pake na pawe ukiwa wala asiwepo mtu atakayekaa humo,’ na, “ ‘Mtu mwingine aichukue nafasi yake.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama vile ilivyoandikwa katika kitabu cha Zaburi, “ ‘Mahali pake na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi humo,’ na, “ ‘Mtu mwingine aichukue nafasi yake ya uongozi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, imeandikwa katika kitabu cha Zaburi: ‘Makao yake yabaki mahame; mtu yeyote asiishi ndani yake.’ Tena imeandikwa: ‘Mtu mwingine achukue nafasi yake ya huduma.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani imeandikwa katika kitabu cha Mashangilio: Kao lake liwe hame tu, asioneke atakayetua mlemle. Tena: Mtu mwingine na autwae ukaguzi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwa sababu imeandikwa hivi katika kitabu cha Zaburi: ‘Makao yake yabakie ukiwa na mutu asiishi ndani yake.’ Na imeandikwa tena: ‘Mutu mwingine atwae kazi yake.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Zaburi, Kikao chake kiwe ukiwa, wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine.