Acts 1:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati alipokutana pamoja nao aliwaamuru hivi: “Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeni ile zawadi aliyoahidi Baba, ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati mmoja Yesu alipokuwa akila pamoja nao, aliwaambia wasiondoke Yerusalemu. Aliwaambia, “Kaeni hapa mpaka mtakapopokea kile ambacho Baba aliahidi kutuma. Kumbukeni, niliwaambia juu yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati walipokutana pamoja aliwaamuru hivi: “Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeeni ile zawadi aliyoahidi Baba, zawadi ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati alipokutana pamoja nao aliwaamuru hivi: “Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeni ile zawadi aliyoahidi Baba, ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke humu Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kutoka kwangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati alipokutana pamoja nao aliwaamuru hivi: “Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeni ile zawadi aliyoahidi Baba, ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuwakusanya akawaagiza, wasitoke Yerusalemu, ila wakingoje kiagio cha Baba, mlichokisikia kwangu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja alipokuwa akikusanyika pamoja nao, akawaagiza: “Musitoke Yerusalema, lakini mubaki kule mukingojea zawadi ambayo Baba yangu aliahidi, ile niliyowaambia ninyi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta, akikutana nao, akawaagiza wasitoke katika Yerusalemi, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia khabari zake kwangu;