Acts 10:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu aliyeitwa Kornelio, aliyekuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kulikuwa mtu aliyeitwa Kornelio katika mji wa Kaisaria. Mtu huyu alikuwa ofisa wa kikosi kilichoitwa “Kikosi cha Kiitalia” katika jeshi la Rumi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, Jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, jemadari wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesaria kulikuwa na mtu, jina lake Kornelio, mkubwa wa kikosi cha askari kilichoitwa cha Italia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika muji Kaisaria, kulikuwa mutu mumoja jina lake Kornelio. Yeye alikuwa mukubwa wa kundi la waaskari lililoitwa “Kundi la Italia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,