Acts 10:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hayo maono aliyokuwa ameyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro alipokuwa akisumbuka kuhusu maana ya maono hayo, wale watu waliotumwa na Kornelio waliipata nyumba ya Simoni, wakasimama kwenye lango.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro alijiuliza maono haya yalikuwa na maana gani. Watu ambao Kornelio aliwatuma walishaiona nyumba ya Simoni na walikuwa wamesimama mlangoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hilo maono alilokuwa ameliona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hayo maono aliyokuwa ameyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati Petro alipokuwa akisumbuka ndani ya nafsi yake, juu ya maana ya maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakatokeza. Walikuwa kukiulizia nyumba ya Simoni, wakiwa wamesimama mbele ya lango,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hayo maono aliyokuwa ameyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Petero alipopotelewa moyoni mwake, asijue maana ya hayo, aliyoyaona, papo hapo wale watu waliotumwa na Kornelio wakasimama mlangoni wakiiuliza nyumba ya Simoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro alipokuwa angali na wasiwasi, naye akijiuliza juu ya maana ya maono yale, wale watu waliotumwa na Kornelio wakafika mbele ya mulango kwa maana walikuwa wamekwisha kujulishwa nafasi gani kunapokuwa nyumba ya Simoni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta Petro alipokuwa akiona mashaka ndani ya nafsi yake, maana yake nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiislia kuiulizia nyumba ya Simon, wakasimama mbele ya mlango,