Acts 10:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye na jamaa yake yote walikuwa wacha Mungu; alitoa kwa ukarimu kwa wale walio na mahitaji na kumwomba Mungu mara kwa mara.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwa mcha Mungu. Yeye na watu wengine wote walioishi katika nyumba yake walikuwa wanamwabudu Mungu wa kweli. Alitoa pesa zake nyingi kuwasaidia maskini miongoni mwa Wayahudi na daima alimwomba Mungu kwa kufuata utaratibu kama ilivyokuwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mwenyezi Mungu daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mtu mtauwa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alimtii Mungu na kumcha pamoja nao wote wa nyumbani mwake: wengi wa kwao aliwagawia vipaji vingi, tena alikuwa akimwomba Mungu po pote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye alikuwa mwenye kuogopa Mungu, naye alimwabudu Mungu pamoja na watu wote waliokuwa kwake. Aliwasaidia wamasikini wengi, naye alikuwa akimwomba Mungu siku zote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.