Acts 10:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani mwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno kwako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale watu wakasema, “Malaika mtakatifu amemwambia Kornelio akualike nyumbani mwake. Ni mtu mwema na hutenda kwa haki, na anamwabudu Mungu na Wayahudi wote wanamheshimu. Malaika alimwambia akualike nyumbani kwake ili asikilize yale utakayosema.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na kamanda Kornelio ambaye ni mtu mwema anayemcha Mungu na kusifiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika wa Mungu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, Kornelio jemadari, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, ili asikilize kile utakachosema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakasema: Kornelio aliye mkubwa wa askari ni mtu mwongofu, mwenye kumcha Mungu, hata wote wa taifa la Wayuda wanamsemea vizuri; huyo ameagizwa na malaika mtakatifu, atume kwako, uje nyumbani mwake, ayasikie, utakayomwambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno kwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakamujibu: “Tumetumwa hapa na Kornelio, mukubwa wa waaskari. Yeye ni mutu wa haki na mwenye kumutii Mungu, naye anasifiwa na Wayuda wote. Malaika mutakatifu amemutokea na kumwagiza akuite ufike kwake kusudi asikie maneno utakayomwambia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.