Acts 10:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Petro akawakaribisha ndani wawe wageni wake. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akawakaribisha ndani watu wale ili walale usiku huo. Siku iliyofuata Petro alijiandaa na kuondoka na wale watu watatu. Baadhi ya waamini katika mji wa Yafa walikwenda pamoja naye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro akawaalika ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, akifuatana na baadhi ya ndugu kutoka Yafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani, akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowakaribisha na kuwafikiza. Kesho yake akainuka, akatoka pamoja nao, hata wengine wa Yope waliokuwa ndugu wakaenda pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Petro akawakaribisha ndani ya nyumba na kuwapangisha mule. Kesho yake Petro akafunga safari pamoja nao. Na wandugu waamini wamoja waliokaa Yopa wakamusindikiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae.