Acts 10:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro akawaambia, “Nyinyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Mnajua kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akawaambia watu wale kuwa, “Mnaelewa kuwa ni kinyume na sheria yetu kwa Myahudi kushirikiana au kumtembelea mtu ambaye si Myahudi. Lakini Mungu amenionyesha kuwa nisimchukulie mtu yeyote kuwa yu kinyume na desturi za Kiyahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na Sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro akawaambia, “Nyinyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu ye yote kuwa najisi au asiye safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali kwa mtu aliye Myahudi ashirikiane na mtu wa taifa lingine wala kumtembelea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro akawaambia, “Nyinyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Ninyi mmejua, ya kuwa mtu wa Kiyuda ana mwiko wa kugandamiana na mtu wa kabila jingine au kumfikia. Lakini Mungu amenionyesha, nisimwazie mtu wo wote, kwamba ni wa mwiko au wa mzio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia: “Ninyi munajua wazi kama katika Sheria ya dini yetu inakatazwa kwa Muyuda kushirikiana na mutu wa taifa lingine wala kumutembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba haifai kumuhesabia mutu yeyote kuwa muchafu wala mutengwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.