Acts 10:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kungaa alisimama mbele yangu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu aliyevaa nguo zilizong’aa akasimama mbele yangu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kornelio akasema, Siku tatu zilizopita, katika saa ii hii, yaani saa tisa, nilikuwa nikisali nyumbani mwangu; nikamwona mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zing'arazo,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, kama saa tisa mchana nilikuwa ninaomba ndani ya nyumba yangu. Ghafla akawepo mtu mmoja amesimama mbele yangu amevaa mavazi meupe yanayong'aa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kun'gaa alisimama mbele yangu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kung'aa alisimama mbele yangu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu mwenye nguo za kumetameta akasimama mbele yangu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu aliyevaa nguo zilizong’aa akasimama mbele yangu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kornelio akasema, Siku tatu zilizopita, katika saa ii hii, yaani saa tisa, nilikuwa nikisali nyumbani mwangu; nikamwona mtu amesimama mbele yangu, akiwa amevaa nguo zinazong'aa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kungaa alisimama mbele yangu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kornelio akasema: Leo ni siku ya nne, tangu nilipokuwa nikifunga mpaka saa hii, tena nikimwomba Mungu nyumbani mwangu, saa tisa ilipofika. Papo hapo mtu alisimama mbele yangu aliyevaa nguo zilizomerimeta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kornelio akasema, Siku tatu zilizopita, katika saa ii hii, yaani saa tisa, nilikuwa nikisali nyumbani mwangu; nikamwona mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zing’arazo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kornelio akajibu: “Kumekwisha kupita siku tatu, mimi nilikuwa nikiomba ndani ya nyumba yangu kwa saa hii hii ya saa tisa ya muchana. Mara moja nikaona mutu anayevaa nguo yenye kungaa sana, akisimama mbele yangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema,