Acts 10:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Yudea na Yerusalemu. Wakamuua kwa kumtundika msalabani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tuliona yote ambayo Yesu alitenda katika Uyahudi na katika mji wa Yerusalemu. Lakini aliuawa. Walimpigilia kwenye msalaba uliotengenezwa kwa mti.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Uyahudi na Yerusalemu. Wakamwua kwa kumtundika msalabani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Uyahudi na Yerusalemu. Wakamuua kwa kumtundika msalabani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nasi tumeyaona yote, aliyoyafanyiza katika nchi ya Wayuda namo Yerusalemu. Huyo walimwangamiza na kumtundika mtini,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sisi tuko washuhuda wa mambo yote Yesu aliyofanya katika inchi ya Wayuda na katika muji wa Yerusalema. Walimwua kwa kumutundika juu ya musalaba,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nasi tu mashahidi ya mambo yote aliyoyatenda katika inchi ya Wayahudi na katika Yerusalemi; ambae walimwua wakamtundika mtini.