Acts 10:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala hatazisahau.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akiwa anashangaa na kuogopa, Kornelio akasema, “Unataka nini, bwana?” Malaika akamwambia, “Mungu amesikia maombi yako na ameona sadaka zako unazowapa maskini. Anakukumbuka kwa yote uliyotenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala hatazisahau.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamkodolea macho, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala hatazisahau.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamkazia macho, akashikwa na woga, akasema: Nini, Bwana? Akamwambia: Maombo yako na magawio yako yamefika juu machoni pa Mungu, anayakumbuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kornelio akamukazia macho akiwa ameshikwa na woga, akamwuliza: “Bwana, ni nini?” Malaika akamujibu: “Mungu amesikia maombi yako na kupendezwa na misaada unayotoa kwa wamasikini, na kwa hiyo anakukumbuka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.