Acts 10:45 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waumini waliokuwa wametahiriwa waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho wa Mungu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waamini wa Kiyahudi waliofuatana na Petro walishangaa kwamba Roho Mtakatifu amemiminwa kama zawadi hata kwa watu wasio Wayahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia zawadi ya Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wa tohara walioamini waliokuwa wamekuja pamoja na Petro walishangaa kuona kuwa kipawa cha Roho Mtakatifu kimemwagwa juu ya watu Mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wa tohara walioamini waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho wa Mwenyezi Mungu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wenye kumtegemea Bwana waliotahiriwa, waliokuja pamoja na Petero, waliposhangaa sana, ya kuwa hata wamaizimu humiminiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wale wanafunzi Wayuda waliofika pamoja na Petro wakashangaa sana kwa kuona kwamba Mungu ametoa zawadi ya Roho wake Mutakatifu kwa watu wa mataifa mengine vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.