Acts 10:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika aliyeongea na Kornelio akaondoka. Ndipo Kornelio aliita watumishi wake wawili na askari mmoja. Askari alikuwa mcha Mungu, mmoja wa wasaidizi wake wa karibu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa kati ya wale waliomhudumia daima;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Malaika aliyesema naye alipokwenda zake, akaita watumishi wawili na askari mwenye kumcha Mungu miongoni mwao walioshikana naye siku zote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule malaika aliyesema na Kornelio alipoondoka, akawaita watu wawili kati ya watumishi wake na askari mumoja mwenye kuogopa Mungu, aliyekuwa mumoja wa wasimamizi wake wa kipekee.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima: