Acts 11:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliposikia haya hawakuwa na lingine la kupinga. Nao wakamsifu Mungu, wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waamini wa Kiyahudi waliposikia hili, wakaacha kubisha. Wakamsifu Mungu na kusema, “Kwa hiyo Mungu anawaruhusu watu wasio Wayahudi kubadili mioyo yao na kuwa na maisha anayotoa!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu na kuwa na uzima!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mwenyezi Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipoyasikia haya wakanyamaza kimya, wakamtukuza Mungu wakisema: Kumbe hata wamizimu Mungu amewapa majuto, nao wapate uzima!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu waamini waliposikia maneno hayo, wakatulia na kumusifu Mungu, wakisema: “Kumbe Mungu amewajalia hata watu wa mataifa mengine vilevile kusudi waweze kugeuka toka zambi na kupata uzima kamili.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.