Acts 11:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini baadhi yao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria Injili kuhusu Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya waamini hawa walikuwa watu kutoka Kipro na Kirene. Watu hawa walipofika Antiokia, walianza kuwahubiri watu wasio Wayahudi. Waliwahubiri Habari Njema kuhusu Bwana Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria ile Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini baadhi yao walikuwapo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakimhubiri Bwana Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kigiriki, wakihubiri Habari Njema za Bwana Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini baadhi ya waumini waliotoka Kupro na Kurene, walikwenda Antiokia wakautangaza huo ujumbe kwa watu wa mataifa mengine wakiwahubiria Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wengine wao walikuwa watu wa Kipuro nao wa Kirene. Hao walipofika Antiokia, wakawapigia hata Wagriki mbiu njema ya Bwana Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kulitokea wanafunzi wengine, waliokuwa watu wa Kipuro na wa inchi ya Kurene, waliofika Antiokia. Nao wakaanza kusemezana na Wagriki vilevile, wakiwahubiri Habari Njema juu ya Bwana Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.