Acts 11:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu na imani. Alipokwenda Antiokia na kuona jinsi Mungu alivyowabariki waamini pale, alifurahi sana. Akawatia moyo wote, akasema, “Iweni waaminifu kwa Bwana daima. Mtumikieni Yeye kwa mioyo yenu yote.” Watu wengi zaidi wakawa wafuasi wa Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mwenyezi Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipofika na kuviona vipaji, Mungu alivyowagawia, akafurahi, akawahimiza wote, wakaze mioyo kushikamana na Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye alipofika, akaona mambo yote yaliyotendeka kutokana na neema ya Mungu, akafurahi, naye akawatia wanafunzi wote moyo kusudi waendelee kushikamana na Bwana kwa moyo wao wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.