Acts 11:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wao aliyeitwa Agabo akasimama, akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu kwamba njaa kubwa ingeenea ulimwengu mzima. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmoja wao, aliyeitwa Agabo, huku akisaidiwa na Roho Mtakatifu, alisimama na kuzungumza. Alisema, “Wakati mbaya sana unakuja katika dunia yote. Hakutakuwa chakula kwa ajili ya watu kula.” (Kipindi hiki cha njaa kilitokea Klaudio alipokuwa mtawala wa Kirumi)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote (Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa akitawala).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao, jina lake Agabo, akainuka kwa kuongozwa na Roho, akaonyesha, kwamba itakuwa njaa kubwa ulimwenguni mote; nayo ikawako siku za Klaudio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mumoja wao, aliyeitwa Agabo, akasimama, akatabiri kwa njia ya Roho Mutakatifu kwamba kutakuwa njaa kubwa katika dunia nzima. (Nayo ikatokea katika nyakati za utawala wa mufalme Klaudio wa Roma.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.