Acts 11:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kutoka mbinguni ikiwa imeshikwa pembe zake nne, ikawekwa kando yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama kitambaa kikubwa kikishuka kutoka mbinguni, kikashushwa kwa ncha zake nne, nacho kikanikaribia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akasema, “Nilikuwa katika mji wa Yafa. Nilipokuwa nikiomba, niliona maono. Niliona kitu kikishuka chini kutoka mbinguni. Kilionekana kama shuka kubwa ikishushwa chini kwa pembe zake nne. Kikaja chini karibu yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa likishushwa chini kutoka mbinguni likiwa limeshikwa pembe zake nne, likawekwa kando yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kutoka mbinguni ikiwa imeshikwa pembe zake nne, ikawekwa kando yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inateremshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kutoka mbinguni ikiwa imeshikwa pembe zake nne, ikawekwa kando yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nilipokuwa katika mji wa Yope nikimwomba Mungu, nikaingiwa na kituko kwa kuona njozi: chombo kinachofanana na guo kubwa linatelemshwa chini toka mbinguni likishikwa kwa pembe zake nne likaja mpaka hapo, nilipokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mimi nilikuwa katika muji Yopa nikiomba. Kisha nikakuwa sawa nimezimia, nami nikapata maono. Nikaona kitu kinachokuwa kama nguo kubwa kikishuka toka mbingu, kikitelemushwa, kikishikwa kwenye pembe zake ine. Nacho kikafika karibu nami.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.