Acts 11:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama mwitu, wanyama watambaao, na ndege wa angani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipotazama ndani yake, niliona aina zote za wanyama, pamoja na wale wa porini, wanyama wanaotambaa na ndege.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwitu, watambaao na ndege wa angani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama wa mwitu, watambaao na ndege wa angani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, wale watambaao, na ndege wa angani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nilipochungulia mle nikitazama, nikaona, mna nyama wenye miguu minne wa nchini nao nyama wa mwituni nao watambao nao ndege wa angani;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipochungulia ndani yake kwa uangalifu, nikaona nyama wa ufugo wenye miguu mine, nyama wa pori, nao nyama wenye kutambaa pamoja na ndege.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaitazama sana, nikifikiri, nikaona nyama za inchi zenye miguu mine, Ua nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga.