Acts 12:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipita kundi la kwanza la walinzi na la pili, wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo, wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro na malaika wakavuka lindo la kwanza na lindo la pili. Kisha walifika kwenye lango la chuma lililowatenganisha na mji. Lango likafunguka. Baada ya kuvuka lango na kutembea umbali wa kama mtaa mmoja, malaika akatoweka ghafla.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipopita kundi la walinzi wa kwanza na wa pili, wakafika hadi mbele ya lango la chuma la kuingilia mjini, nalo lango likawafungukia lenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipita kituo cha kwanza cha ulinzi na cha pili, halafu wakafika kwenye mlango wa chuma wa kuingilia mjini. Huo mlango ukawafungukia wenyewe, nao wakatoka nje. Wakawa wanatembea katika barabara moja na mara yule malaika akamwacha Petro peke yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakapita zamu ya kwanza ya walinzi na ya pili, wakalifikia lango la chuma linaloelekea mjini, nalo likawafungukia lenyewe, wakatoka; walipoendelea njia tu, papo hapo ndipo, malaika alipoondoka na kumwacha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakapita kikundi cha kwanza cha waaskari na cha pili, na kufikia kwenye mulango wa chuma wa kuingilia ndani ya muji. Ule mulango ukajifungua wenyewe mbele yao, nao wakatoka inje na kuendelea katika barabara moja. Na kwa rafla yule malaika akamwacha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hatta mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia. Wakatoka, wakapita katika njia moja; marra malaika akamwacha.