Acts 12:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa mikononi mwa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yoyote kuwa Mwenyezi Mungu amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka makucha ya Herode Agripa na kutoka matazamio yote ya Wayahudi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Petro akatambua kuwa haikuwa ndoto. Akawaza moyoni akisema, “Sasa ninajua kwamba Bwana hakika alimtuma malaika wake kwangu. Ameniokoa kutoka kwa Herode na kutoka kwenye mabaya yote ambayo Wayahudi walidhani yatanipata.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa kutoka katika mkono wa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa mikononi mwa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yo yote kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka katika makucha ya Herode Agripa na kutoka katika matazamio yote ya Wayahudi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yoyote kuwa Mwenyezi Mungu amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka makucha ya Herode Agripa na kutoka matazamio yote ya Wayahudi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua hakika kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo ndipo Petro alipotambua yaliyotukia, akasema, “Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana amemtuma malaika wake akaniokoa mikononi mwa Herode na kutoka katika mambo yale yote watu wa Israeli waliyotazamia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Petero, moyo wake ulipomrudia, akasema: Sasa nimejua kweli ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake, akaniokoa katika mkono wa Herode na katika mangojeo yote ya watu wa kwao Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro alipotambua kwamba mambo yaliyotokea ni ya kweli akasema: “Sasa ninajua hakika kwamba Bwana alimutuma malaika wake kuniokoa katika mikono ya Herode na katika mabaya yote Wayuda waliotaka kunitendea.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi.