Acts 12:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Mwenyezi Mungu alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akawafanyia ishara kwa mkono wake kuwaambia wanyamaze. Akawaeleza namna Bwana alivyomtoa nje ya gereza. Akasema, “Mwambieni Yakobo na ndugu wengine kilichotokea.” Kisha akawaacha na kwenda sehemu nyingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Mwenyezi Mungu alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka, akaenda sehemu nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro aliwaashiria kwa mkono wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Kisha akawaambia watoe taarifa ya jambo hilo kwa Yakobo na wale ndugu wengine, halafu akatoka akaenda mahali pengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawapungia mkono, wanyamaze; kisha akawasimulia, jinsi Bwana alivyomtoa kifungoni, akasema: Habari wapasheni nao akina Yakobo nao walio ndugu! Kisha akatoka, akaenda mahali pengine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akawanyamazisha kwa kunyoosha mukono, kuwaelezea namna Bwana alivyomwondoa katika kifungo. Akawaambia tena: “Muwaelezee Yakobo na wandugu wengine waamini habari hizi.” Kisha Petro akaondoka na kwenda nafasi ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.