Acts 12:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipopambauka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata askari walichanganyikiwa. Walijiuliza nini kimempata Petro.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale maaskari kuhusu yaliyomtukia Petro.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa juu ya yaliyompata Petro.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipokucha, ulitokea wasiwasi mkubwa kati ya wale askari kuhusu yaliyokuwa yamempata Petro.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palipokucha, pakapatikana mahangaiko mengi kwa askari, wasijue, jinsi ya Petero yalivyowezekana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipopambauka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha, waaskari wakapigwa na hofu sana. Wakaanza kuulizana: “Jambo gani lililomupata Petro?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro.