Acts 12:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea, akaenda Kaisarea ambako alikaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwauliza-uliza wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akatelemkia kutoka Uyahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Herode alimtafuta kila mahali lakini hakumpata. Hivyo aliwahoji walinzi na kuamuru wauawe. Baadaye, Herode alihama kutoka Uyahudi na kwenda katika mji wa Kaisaria na kukaa huko kwa muda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea akaenda Kaisarea ambako alikaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea, akaenda Kaisarea ambako alikaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwahoji wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akateremka kutoka Yudea kwenda Kaisaria, akakaa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Herode aliamuru ufanywe msako lakini hawakuweza kumpata. Hivyo aliamuru wale askari wahojiwe, akatoa amri wauawe. Halafu akatoka huko Yudea, akaenda Kaisarea ambako alikaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Herode asipompata hapo, alipomtaka, akawaulizauliza walinzi, akaagiza, wafungwe. Kisha akaondoka Yudea, akatelemka kwenda Kesaria, akatua huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwauliza-uliza wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akatelemkia kutoka Uyahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Herode akaomba wamutafute, lakini hawakumwona. Kwa hiyo kisha kusambisha wale walinzi, akaamuru wauawe. Halafu Herode akaondoka Yudea kwenda katika muji Kaisaria na kukaa kule kwa muda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Herode alipomtafuta, asimwone, akawauliza walinzi, akaamuru wanawe. Nae akatelemka kutoka Yahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko.