Acts 12:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Mwenyezi Mungu akampiga, naye akaliwa na chango, akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Herode hakumpa Mungu utukufu. Hivyo malaika wa bwana akampiga kwa ugonjwa. Akaliwa na minyoo ndani na kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula, kwa kuwa Herode Agripa hakumpa Mungu utukufu, malaika akampiga, akaliwa na chango akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Mwenyezi Mungu akampiga, naye akaliwa na chango, akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
papo hapo malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. Akawa akiliwa na vidudu, akakata roho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na pale pale malaika wa Bwana akamwazibu Herode kwa ugonjwa kwa sababu alijitukuza kwa pahali pa Mungu. Herode akakuliwa na michango ya tumbo na kisha akakufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu: akaliwa na funza, akatoa roho.