Acts 12:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipoona kuwa kitendo hicho kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata Petro pia. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Herode alipoona kuwa Wayahudi wamelifurahia jambo hili, aliamua kumkamata Petro pia. Hii lilitokea katika kipindi cha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipoona kuwa kitendo hiki kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipoona kuwa kitendo hicho kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi aliendelea na kumshika Petro pia. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipoona kuwa kitendo hicho kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoona, ya kuwa Wayuda wamependezwa, akaendelea, akamkamata naye Petero, siku za mikate isiyochachwa zilipotimia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, alipoona kwamba jambo lile liliwapendeza Wayuda, akaamuru Petro afungwe vilevile. (Mambo haya yalitokea kwa wakati wa sikukuu ya Mukate Usiotiwa Chachu.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamtwaa na Petro. Siku hizo ndizo siku za mikate isiyochachwa.