Acts 12:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kumkamata alimfunga gerezani chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alimkamata Petro na kumfunga gerezani, ambako alilindwa na kundi la askari kumi na sita. Herode alipanga kumleta Petro mbele ya watu ili ahukumiwe, lakini alisubiri mpaka baada ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kutiwa nguvuni, Petro alifungwa gerezani, akawekwa chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari wannewanne. Herode alikusudia kumtoa hadharani baada ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kumkamata akamtia kifungoni, akaagiza vikosi vinne, kila kikosi cha askari wanne, wamlinde kwa zamu, akataka kumtia mikononi mwa watu, siku za Pasaka zitakapokuwa zimepita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokwisha kumukamata Petro, na kumutia katika kifungo, akamuweka chini ya ulinzi wa vikundi vine vya waaskari waliogomboana wane kwa wane. Naye alikusudia kumusambisha mbele ya watu nyuma ya sikukuu ya Pasaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa askari wanewane, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa mbele ya watu.