Acts 12:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda lango la gereza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wa usiku kabla ya siku ambayo Herode alipanga kumhukumu mbele ya watu, Petro, akiwa amefungwa minyororo miwili, alikuwa amelala katikati ya askari wawili. Na askari waliokuwa nje ya mlango walikuwa wanalinda gereza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakalilinda gereza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usiku, kabla ya siku ile ambayo Herode angemtoa Petro hadharani, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa minyororo miwili, na walinzi walikuwa wanalinda lango la gereza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo, Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule Petero alikuwa amelala katikati ya askari wawili akiwa amefungwa na mapingu mawili; nao walinzi walikilinda kifungo mlangoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku, mbele ya kutimia kwa siku Herode aliyotaka kumusambisha mbele ya watu, Petro alikuwa amelala ndani ya chumba katikati ya waaskari wawili. Alikuwa amefungwa na minyororo miwili, nao walinzi walikuwa wakichunga mulango wa kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.