Acts 12:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa ubavuni akamwamsha akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo iliyomfunga mikono ikakatika na kuanguka chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula malaika wa Mwenyezi Mungu akatokea, na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ghafla malaika wa Bwana alikuwa amesimama pale, na chumba kilijaa mwanga. Malaika akamwamsha Petro kwa kumpiga upande, akasema, “Amka haraka!” Minyororo ikaanguka kutoka mikono mwa Petro.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa akisema, “Amka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka katika mikono yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa ubavuni akamwamsha akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo iliyomfunga mikono ikakatika na kuanguka chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula malaika wa Mwenyezi Mungu akatokea, na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghafla, malaika wa Bwana akasimama karibu naye na mwanga ukaangaza kile chumba cha gereza. Malaika akamgusa ubavuni akamwamsha akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo iliyomfunga mikono ikakatika na kuanguka chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara malaika wa Bwana akasimama hapo karibu, nao mwanga ukamulika chumbani. Akamwamsha Petero kwa kumpiga ubavu akisema: Inuka upesi! Ndipo, mapingu yalipomwanguka mikononi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa rafla malaika wa Bwana akatokea na mwangaza ukajaa ndani ya chumba kile. Malaika akamutikisa Petro na kumwamusha, akimwambia: “Simama upesi!” Nayo minyororo ikaanguka toka kwenye mikono yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka.