Acts 12:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo malaika akatoka nje na Petro alimfuata. Hakujua kama kweli malaika alikuwa anafanya hili. Alidhani alikuwa anaona maono.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro alitoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro akamfuata nje lakini hakujua kama hayo yaliyofanywa na huyo malaika yalikuwa ya kweli; alidhani alikuwa anaota ndoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatoka akimfuata, asijue, kama ni kweli yaliyofanyika na malaika; maana aliwaza, ameona njozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro akamufuata mpaka inje ya kifungo. Lakini hakutambua kwamba mambo yale malaika aliyofanya yalikuwa ya kweli; alizani kwamba amepata maono.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatoka, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni khabari ya kweli iliyofanyika na malaika; bali alidhani anaona njozi.