Acts 13:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa mwaamini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Gavana alipoyaona haya, akaamini. Akayashangaa mafundisho kuhusu Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa muumini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa mwaamini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo yule mtawala, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mkuu wa kisiwa alipoona hayo, aliongoka akawa mwaamini; akastaajabia sana mafundisho aliyosikia juu ya Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtawala nchi alipoyaona yaliyofanyika, akaustaajabu huo ufundisho wa Bwana, akamtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule liwali alipoona mambo yale yaliyotokea, akashangaa na mafundisho ya Bwana hata akapata kumwamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.