Acts 13:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Torati ya Musa na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria ya Musa na maandishi ya manabii vilisomwa. Kisha viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe Paulo na Barnaba, wakisema, “Ndugu zetu, ikiwa mna kitu chochote cha kusema kitakachowasaidia watu hapa, tafadhali semeni.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya masomo katika kitabu cha Sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kusomwa Torati na vitabu vya manabii, viongozi wa lile sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwasaidia watu hawa, tafadhali lisemeni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Torati ya Musa na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, baada ya Torati na kitabu cha Manabii kusomwa, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mafungu ya Maonyo na ya Wafumbuaji yalipokwisha kusomwa, wakubwa wa nyumba ya kuombea wakatuma kwao kwamba: Ndugu zetu, mkiwa na neno la kuituliza mioyo ya watu lisemeni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na nyuma ya kusoma katika vitabu vya Sheria na vya manabii, wakubwa wa ile nyumba ya kuabudia wakatuma mutu kwa kuwaambia: “Wandugu, ikiwa muko na maneno ya kuwatia watu moyo, muyaseme.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.